IQNA

Imamu wa msikiti wa Washington:

Ubeberu na Uzayuni ndio changamoto kubwa zaidi ya Waislamu

19:31 - March 16, 2009
Habari ID: 1756701
Ubeberu na Uzayuni ndio msingi wa changamoto zote na matatizo yanayowakabili Waislamu na kunahitajika umoja na mshikamano wa Kiislamu ili kuweza kushinda makundi hayo.
Hayo yamesemwa na Imamu wa swala za jamaa wa msikiti wa Washington Muhammad al Asi ambaye ameongeza kuwa, Waislamu kote ulimwengu daima wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na madola ya kibeberu na ya mabavu, na utegemezi wa kiuchumi, kiteknolojia na katika masuala ya kijeshi. Amesema kuwa changamoto hizo zimesababisha matatizo mengi kwa Waislamu.
Sheikh Muhammad al Asi amesema kuwa changamoto nyingine zinazowakabili Waislamu ni pamoja na hamu ya baadhi ya nchi za Kiislamu ya kutaka kujiunga na Umoja wa Ulaya au kuwa mwanachama katika jumuiya za Kimagharibi, mafunzo yanayotolewa na nchi adui kwa majeshi ya nchi za Kiislamu, vituo vya kijeshi vya nchi za Magharibi katika nchi za Kiislamu na mtindo wa baadhi ya nchi za Kiislamu wa kununua silaha na zana za kijeshi za kale kutoka nchi za kibeberu na Wazayuni.
Amesema kuwa Ubeberu na Uzayuni ndio mama wa changamoto na matatizo yote. Amesisitiza kuwa Wazayuni na mabeberu wa Kimagharibi wanafanya njama mchana na usiku na kwa njia mbalimbali kama kuzusha hitilafu na mifarakano kati ya Waislamu ili kuzuia maendeleo yao katika nyanja mbalimbali za kijeshi, kiuchumi na kisiasa.
Imamu wa msikiti wa Washington amesema kuwa Waislamu wanapaswa kumtambua vyema adui wao wa pamoja na kuungana katika kukabiliana nae. Amesisitiza kwamba haijuzu kwa Waislamu kuwaruhusu maadui zao wazikalie kwa mabavu ardhi tukufu, kushambulia nchi za Kiislamu, kupora maliasili zao na kuanzisha vituo vya kijeshi katika nchi za Kiislamu.
Sheikh Muhammad al Asi ameashiria juhudi za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika nyanja mbalimbali hususan katika kukabiliana na Uzayuni na ubeberu na akasema, katika miaka ya hivi karibuni Iran ya Kiislamu imeonyesha ikhlasi katika kutatua matatizo ya Waislamu hususan kadhia ya Quds Tukufu na Palestina inayokaliwa kwa mabavu. 378016
captcha