Akizungumza hivi karibuni pambizoni mwa kikao cha kimataifa cha 22 cha Umoja wa Kiislamu mjini Tehran, Swadrudeen Qubanchi, Imamu wa Ijumaa wa mji mtakatifu wa Najaf ahuko Iraq mesema kuwa wananchi wa Iraq wameweza kuleta mabadiliko makubwa ya kihistoria nchini humo kupitia uchaguzi uliofanyika hivi karibuni nchini, ambapo wameweza kudhihirisha misimamo ya pamoja ya kisiasa ya wafuasi wa Kisuni na Kishia nchini humo. Amesema, wananchi wa nchi hiyo wamesimama kidete dhidi ya uvamizi wa Marekani na kwamba nchi hiyo ambayo iliivamia Iraq kwa kisingizio cha kuiletea demokrasia na uhuru, hivi sasa yenyewe imekwama katika matatizo makubwa nchini humo.
Ameashiria baadhi ya mafanikio makubwa yaliyopatikana nchini kuwa ni pamoja na kufanyika chaguzi mbalimbali za kupigania kujitawala kisiasa, kumaliza ukaliwaji mabavu wa nchi, kukomeshwa vita vya ndani na kupitishwa kwa katiba ya nchi hiyo ya Kiislamu.
Qubanchi ameashiria idadi kubwa ya Mashia waliofanya ziara hivi karibuni katika makaburi na maeneo matakatifu huko katika mji wa Samarra na kuongeza kuwa licha ya kuwa mji huo ni wa Kisuni, lakini wakazi wake waliwakaribisha kwa moyo mkunjufu Waislamu wenzao wa madhehebu ya Shia na hata baadhi yao kuwakaribisha kwenye nyumba zao wageni wao wa Kishia baada ya kuadimika hoteli katika mji huo. Amesema Umoja unapasa kusakwa ili uthibiti. 378506