Huku akiashiria usomaji Qur'ani wa Mustafa Ismail, mmoja wa wasomaji wa kimataifa wa Qur'ani wa Iran amesema kuwa, usomaji Qur'ani wa marehemu Mustafa Ismail uko katika kilele cha juu zaidi cha usomaji wa kitabu hicho kitakatifu na kwamba, hata wale wasomaji mashuhuri wanaomuiga msomaji huyo mashuhuri wa Misri wangali nyuma sana wakilingalishwa naye katika usomaji.
Hayo yamesema na Swalah At'harifard, msomaji wa Qur'ani wa kimataifa wa Iran katika mazungumzo yake na Shirika la Kimataifa la Habari za Qur'ani IQNA.
Amesema kuwa wasomaji wote wa Qur'ani waliokuja baada ya Mustafa Ismail, akiwemo Abdul Basit, ambaye inaonekana kuwa anaiga kwa njia maalumu usomaji wa Muhammad Rafat, walinufaika mno na usomaji wa Ustadh Mustafa Ismail, ambapo wanasikika wakisoma kwa lahani maalumu ya marehemu ustadh huyo.
Swalah At'harifard amesema, sifa muhimu ya usomaji wa Ustadh Mustafa Ismail ni usomaji wake ulioandamana na uzingatiaji wa maana ili kumfahamisha na kumuathiri msikilizaji, jambo ambalo tunaona likizingatiwa pia na wasomaji wa zama hizi wa Qur'ani. 374191