Mpango huo wa kidini na kiutamaduni umeanza kutekelezwa kutokana na pendekezo la Rais Abdul Aziz Butefliqa na kwa ushirikiano wa Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kidini ya nchi hiyo. Pambizoni mwa wiki hiyo ya Qur'ani, shughuli mbalimbali za utamaduni, sanaa na maonyesho ya sanaa ya kaligrafia pamoja na vitabu vinavyohusiana na masuala ya Qur'ani yatafanyika ambapo wapenzi wengi wa masuala ya Qur'ani wataruhusiwa kuyatembelea. 379051