IQNA

Amir wa Makka: Uislamu ni dini ya maendeleo na ustawi

10:50 - March 19, 2009
Habari ID: 1757547
Khalid al-Faisal, Amir wa mji mtakatifu wa Makka amesema kuwa Uislamu ni dini ya maendeleo, ustawi, ustaarabu, uadilifu, usawa na uhuru.
Kwa mujibu wa ArabNews, Amir Faisal ameyasema hayo katika hadhara ya wanachuo wa Chuo Kikuu cha Mfalme Abdul Aziz mjini Jeddah na kukosoa propaganda chafu zinazoendeshwa na nchi za Magharibi dhidi ya Uislamu kwamba thamani za dini hii tukufu ni chanzo cha kubaki nyuma Waislamu kimaendeleo.
Amir Faisal ambaye alikuwa akizungumzia umuhimu wa misimamo ya wastani katika Uislamu ameongeza kuwa, misimamo hiyo ndicho kipimo cha maisha bora ya Uislamu.
Hotuba hiyo ni sehemu ya hotuba na vikao vya mara kwa mara ambavyo vimekuwa vikifanywa na kiongozi huyo tokea mwanzoni mwa mwaka huu. 379546
captcha