IQNA

Atlasi ya Qur'ani yachapishwa

10:58 - March 19, 2009
Habari ID: 1757549
Atlasi ya Qur'ani Tukufu ambayo imeandaliwa na Dakta Shauqi Abu al-Khalil ikiwa na kurasa 240 imechapishwa kwa njia ya kuvutia sana.
Atlasi hiyo inaashiria sehemu za matukio yaliyotajwa kwenye Qur'ani, sehemu yanapoishi makabila mbalimbali na pia maeneo ya kijografia ya matukio yaliyotokea katika maisha ya Mitume wa Mwenyezi Mungu, akiwemo Mtume Muhammad (saw).
Atlasi hiyo pia inagusia maeneo muhimu ya kihistoria yaliyotajwa katika Qur'ani Tukufu ikiwemo sehemu ilipotua safina au jahazi ya Nabii Nuh (as), pango la As'habul Kahf, sehemu ya makazi ya Madyan na sehemu nyinginezo muhimu katika historia ya Kiislamu.
Atlasi hiyo itasaidia pakubwa katika kuondoa utata kuhusu baadhi ya masuala ya kijografia yasiyofahamika vyema katika ulimwengu wa Kiislamu.
Miongoni mwa maeneo yasiyojulikana vyema na Waislamu na ambayo yametajwa na kuashiriwa kwa uwazi mkubwa katika atlasi hiyo ni kama vile sehemu ya Ya'juj na Ma'juj, Swabiun, Bani Qainuqaa, Khaibar na ukombozi wa Makka. 379607
captcha