Msomaji wa Qur'ani raia wa Tanzania aliyeshiriki katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani na hadithi yaliyoandaliwa hivi karibuni na Jamuiya ya Kimataifa ya al-Mustafa (saw) amesisitiza kwamba mashindano ya kimataifa ya Qur'ani yanayoandaliwa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yamepelekea Wasuni na wananchi wa nchi nyinginezo duniani kubadili msimamo na mtazamo wao kuhusiana na Iran na Waislamu wa madhehebu ya Shia.