IQNA

Mwanazuoni wa Kiislamu wa Kishia atiwa nguvuni Saudi Arabia

11:08 - March 19, 2009
Habari ID: 1757587
Askari usalama wa Saudi Arabia wamemtia nguvuni Hujjatul Islam Namir Baqir Namir ambaye ni mwanaharakati wa Kiislamu wa Kishia akiwa njiani kwenda kutekeleza swala ya alfajiri msikitini.
Kituo cha habari cha Khaima kimeripoti kuwa Hujjatul Islam Namir Baqir alitiwa nguvuni na askari usalama mapema alfajiri akiwa njiani kwenye msikitini kutekeleza swala ya alfajiri.
Vyombo vya kuaminika vimesema kuwa magari kadhaa ya askari usalama wa Saudia yalilizingira gari la mwanazuoni huyo na kumtia nguvuni.
Miaka miwili iliyopita pia Sheikh Namir Baqir alikamatwa, kupigwa na kusailiwa na askari usalama wa Saudi Arabia katika mji wa Awamiyya huko mashariki mwa nchi hiyo.
Mwanazuoni huyo ni miongoni mwa wanazuoni wa Kiislamu wa Kishia nchini Saudia ambao mwaka jana waliitaka serikali ya Riyadh kujenga upya makaburi ya Watu wa Nyumba Tukufu ya Mtume (saw) na masahaba zake katika eneo la Baqi' mjini Madina.
Mwanazuoni huyo pia ameitaka serikali ya Saudi Arabia kusaidia ujenzi wa misikiti na vituo vya kidini vya Waislamu wa Kishia. 379233
captcha