Tovuti ya Europenews imeripoti kuwa uchunguzi uliotayarishwa na wataalamu wa Chuo Kikuu cha Arhos nchini Denmark umeonyesha kuwa idadi ya makundi ya Kiislamu imeongeza katika miaka ya hivi karibuni kutoka makundi 14 hadi 57. Ripoti hiyo imesema kuwa, idadi ya watu wanaohudhuria misikitini nchini humo pia imeongezeka kwa kiwango cha kuzingatiwa.
Lenneh Cohller, mtaalamu wa masuala ya jamii wa Denmark ambaye pia ameshiriki katika utafiti wa kundi hilo amesema kuwa sababu ya ongezeko hilo kubwa la makundi rasmi ya Kiislamu ni marekebisho ya sheria zinazohusiana na raia wa kigeni yaliyofanyika mwaka 2004 na kuondolewa vikwazo vya viza kwa wahubiri wa kidini.
Amesema kuwa huko nyuma ilikuwa vigumu mno kwa wahubiri wa kidini kupata viza ya kuingia nchini Denmark.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Waislamu wa Denmark Zuhair Hussein amethibitisha habari hiyo na kusema kuwa kuna mpango wa kupeleka Waislamu wa Denmark katika nchi za kigeni kwa ajili ya kupata elimu na maarifa ya Kiislamu na mafunzo ya uimamu kwa ajili ya misikiti ya nchi hiyo. Amesema kuwa suala hilo litapunguza idadi ya maimamu kutoka nje ya nchi. 379605