Wahifadhi Qur'ani wa Kiirani wanahifadhi hata nambari za aya, idadi ya aya za sura husika, ukurasa na mambo mengineyo, suala ambalo limewashangaza watu wengi.
Hayo yamesemwa na msomaji Qur'ani wa Guinea Conakry Ahmad Hafidh anayeshiriki katika mashindano ya Qur'ani na hadithi ya Jumuiya ya Kimataifa ya Mustafa nchini Iran. Amesema kuwa amehifadhi Qur'ani nchini kwao na kwamba alishiriki pia katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani mjini Tehran mwaka 2005.
Ahmad Hafidh amesisitiza kwamba Wairani wanaipenda mno Qur'ani na Mtume Muhammad (saw) na wanajishughulisha mno na masuala hayo.
Mwafrika huyo aliyehifadhi Qur'ani nzima amesema kuwa amekubali madhehebu ya Kiislamu ya Shia baada ya kufanya utafiri wa muda mrefu na kueleza kuwa nchi ya Guinea Conakry ni nchi ya Kiislamu ambako Waislamu wa Shia wanaunda karibu asilimi 15 ya jamii ya raia wa nchi hiyo.
Ahmad Hafidh amesema, mashindano ya kitaifa ya Qur'ani hufanyika kila mwaka nchini Guinea Conakry yakiwashirikisha wasomaji mashuhri wa Qur'ani. Amesisitiza kuwa mashindano hayo yamekuwa yakifanyika kwa zaidi ya miaka 25 sasa.
Msomaji huyo wa Qur'ani amesema kuwa anashangazwa mno na uhodari wa makarii wa Iran ambao amesema wanahifadhi hata idadi ya aya za Qur'ani, nambari zake, nambari ya ukurasa wa aya inayosomwa na kadhalika. 377889