IQNA

Serikali ya Morocco yazidisha ukandamizaji dhidi ya Waislamu wa Kishia

15:50 - March 26, 2009
Habari ID: 1758090
Serikali ya Morocco imeanzisha wimbi jipya la kuwakandamiza Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini humo.
Shirika la habari la Associated Press limeripoti kuwa serikali ya Morocco imezidisha operesheni ya kuwakamata raia wa maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo kwa tuhuma ya kukubali madhehebu ya Kiislamu ya Kishia.
Mapema wiki hii serikali ya Rabat ilifunga shule moja ya Wairaqi nchini humo kwa madai kwamba inaeneza madhehebu ya Shia.
Jumuiya ya Kutetea Haki za Binadamu ya Morocco imetangaza kuwa hatua hizo zinakwenda kinyume na harakati ya kuelekea kwenye demokrasia na haki za kijamii.
Siku kadhaa zilizopita serikali ya Morocco ilikata uhusiano wake wa kidiplomasia na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kile ilichodai inaeneza madhehebu ya Shia nchini humo. 380224
captcha