IQNA

Kituo kipya cha uhakiki wa Kiislamu kufunguliwa Uholanzi

13:50 - March 29, 2009
Habari ID: 1758687
Waziri wa Elimu wa Uholanzi amesema kuwa atatenga bajeti ya Euro milioni mbili na nusu kwa ajili ya kuasisi kituo cha utafiti wa Kiislamu ISIS.
Habari zinasema kuwa lengo la kuasisiwa kituo hicho ni kushiriki katika masuala ya elimu na uhakiki wa kisayansi wa kimataifa kuhusu dini ya Kiislamu na kuimarisha mijadala ya kimantiki kuhusu kadhia hiyo.
Kituo cha ISISI ni nakala iliyofanyiwa marekebisho ya kituo cha ISIM kilichoasisiwa mwaka 1998 katika mji wa Leyden nchini Uholanzi.
Kituo cha ISISI kitachunguza pia ustawi wa masuala ya kijamii, kisiasa na kiutamaduni cha jamii za kisasa za Kiislamu.
Vyuo vikuu vinne vya Uholanzi vitashirikiana na kituo hicho katika masuala ya utafiti wa Kiislamu.
Gharama za kuendesha kituo hicho kwa kipindi cha miaka mitatu ya awali zitatolewa na Chuo Kikuu cha Leyden. 380822
captcha