Kikao hicho kinahudhuriwa na wawakilishi wa nchi za Misri, Imarati, Mauritania, Saudi Arabia na Kuwait.
Wanafikra, wataalamu na wakuu wa vituo vya wakfu katika nchi za Kiislamu na Kiarabu wanaoshiriki katika kikao hicho wanachunguza na kubadilishana mawazo kuhusu masuala ya wakfu.
Kikao hicho kinafanyika kwa lengo la kuimarisha nafasi ya wakfu na kuratibu juhudi za nchi za Kiislamu katika uwanja huo.
Hii ni mara ya kwanza kwa kikao cha kuchungua masuala ya wakfu kufanyika nje ya Kuwait.
Kikao hicho kinafanyika Morocco katika hali ambayo nchi hiyo imeshindwa kushughulikia suala muhimu zaidi la kukurubisha pamoja madhehebu mbalimbali za Kiislamu. Si hayo tu, bali hivi karibuni Morocco ilianzisha wimbi jipya la kuwakandamiza Waislamu wa madhehebu ya Shia kwa kisingizio cha kukabiliana na hujuma zinazodhoofisha thamani za kidini.
Jumuiya za kutetea haki za binadamu pia zimesema kuwa serikali ya Rabat imezidisha vitendo vya kuwatia nguvuni watu kwa tuhuma za kufuata madhehebu ya Kiislamu ya Kishia. 381331