Abu Shir amesema kuwa Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya serikali halalai ya Hamas huko Palestina inapanga mikakati ya kufungua kanali ya televisheni ya satalaiti ya Qur'ani Tukufu.
Twalib Abu Shair ambaye alikuwa kihutubia hadhara ya Jumuiya ya Marekebisho ya Redio Qur'ani ameashiria matatizo mbalimbali yanayoikabili redio hiyo na akasema kuwa matangazo yake yanafika katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na maeneo ya kusini mwa Sinai huko Misri.
Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kiislamu wa Palestina amesema kuwa Redio Qur'ani imetayarisha ratiba mpya ambazo zinajumuiya vipindi kuhusu Quds Tukufu na na msikiti wa al Aqsa. 382140