IQNA

Isesco kushiriki katika kikao cha mashirika ya OIC

12:34 - April 04, 2009
Habari ID: 1759947
Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Nchi za Kiislamu OIC, litashiriki katika kikao cha ushirikiano wa mashirika na taasisi nyingine za misaada na masuala ya kitaalamu za umoja huo wa Kiislamu.
Kwa mujibu wa Isesco, kikao hicho kitafanyika tarehe 7 na 8 mwezi huu wa Aprili katika makao makuu ya OIC huko Jeddah Saudi Arabia. Masuala yanayohusiana na jinsi ya kutekelezwa mpango wa miaka kumi kwa ajili ya kukabiliana na changamoto za ulimwengu wa Kiislamu katika karne ya 21 yatajadiliwa.
Muhammad Qamari, Mkuu wa Idara ya Uhusiano wa Kigeni na Ushirikiano wa Isesco pia atashiriki katika kikao hicho, ambapo atatoa ripoti kuhusiana na shughuli zilizotekelezwa na Isesco katika kipindi cha mwaka 2008 na pia zinazotazamiwa kufanywa katika mwaka huu wa 2009.
Mpango wa miaka kumi wa OIC ulipitishwa mwaka 2005 katika kikao cha tatu cha dharura huko katika mji mtakatifu wa Makka. Mbali na mpango huo wa miaka 10 Isesco pia imekuwa ikitekeleza miradi ya umoja wa OIC tokea mwaka 2006 hadi 2015.
Inasemekana kuwa tokea mwaka 2006 hadi 2008 Isesco imetekeleza zaidi ya miradi 600 ya bajeti ambayo imezihifadhia nchi na jamii za Kiislamu katika nchi za Magharibi zaidi ya dola milioni 30. 382104
captcha