Kwa mujibu wa Islamonline, wanazuoni na wanafikra kutoka nchi 14 za Kiislamu wanashiriki katika kikao hicho cha siku nne ambacho kinajadili masuala mbalimbali ya ulimwengu wa Kiislamu, likiwemo suala la athari za sheria za Kiislamu katika zama tofauti.
Kikao hicho kinachofanyika katika Msikiti wa Sultan Qabus kinachunguza makala 36 za utafirti zilizowasilishwa na maulamaa, wasomi, wanafikra na wataalamu wa masuala ya Kiislamu.
Khalid Mushrifi, Mkuu wa Ofisi ya Vyombo vya Habari ya Wizara ya Wakfu ya Oman amesema kuwa lengo la kufanyika kikao hicho ni sisitizo juu ya kuzingatiwa zama katika utoaji wa fatuwa za kukidhi mahitaji ya jamii. Ameongeza kuwa masuala ya zama hayapasi kuzingatiwa kwa madhara ya misingi ya sheria za Kiislamu.
Kikao hicho kitaendelea hadi siku ya Jumanne tarehe 7 Aprili. 382922