Shughuli za wiki hii zimeandaliwa na Jumuiya ya Kiislamu ya Chuo Kikuu cha Harvard kwa lengo la kuarifisha Uislamu sahihi na kuondoa fikra potofu kuhusiana na mafundisho ya dini hii tukufu. Katika kipindi cha wiki hii nzima itakayomalizika tarehe 21 Ijumaa, jumuiya hiyo ina lengo la kutekeleza mipango kadhaa ya kuwafundisha watu wasiokuwa Waislamu mafundisho sahihi ya Uislamu.
Rataiba kama vile za kuadhini na kusoma Qur'ani katika nyakati za mapumziko kati ya vipindi vya masomo, mazungumzo kuhusu Uislamu nchini China, picha za Beitul Muqadds katika karne ya 19, swala ya Ijumaa, kuyafahamu mashairi ya Kiislamu ambayo yametarjumiwa katika zaidi ya lugha 10, maonyesho ya vitabu vya Kiislamu ni miongoni mwa ratiba zitakazotekelezwa katika wiki hiyo. 382952