IQNA

Wachapishaji, wahusika wa makosa ya chapa katika Qur'ani

14:06 - April 07, 2009
Habari ID: 1761411
Muhammad al-Masrawi, Mkuu wa Jumuiya ya Kuchunguza Qur'ani katika Chuo Kikuu cha al-Azhar nchini Misri ameashiria makosa ya chapa yanayofanywa mara kwa mara katika uchapishaji wa kitabu kiakatifu cha Qur'ani na kusisitiza kwamba mashirika ya chapa yanayofanya makosa hayo ndio wahusika wakuu wanaopaswa kubebeshwa jukumu la makosa hayo.
Kwa mujibu wa tovuti ya Muhit, Ahmad al-Masrawi amesema kuwa hakuna makosa makubwa na ya kimsingi yanayoonekana katika uchapishaji wa kitabu hicho lakini kwamba makosa madogomadogo yanayofanywa kuhusiana na suala hilo yanatokana na uzembe unaofanywa na mashirika ya uchapishaji.
Amesema suala hilo linahusiana na masuala ya kibiashara moja kwa moja na kwamba kama mashirika hayo yangekuwa angalifu kidogo, makosa kama hayo yasingelitokea.
al-Masrawi amewataka wahusika kutoa mashinikizo dhidi ya mashirika hayo ili kutokaririwa makosa kama hayo ya chapa katika kitabu hicho cha wahyi. Amesema, kuna sheria za kuwaadhibu wahalifu wanaohusika na makosa kama hayo katika Baraza la Taifa la Misri na kwamba katika siku zijazo sheria hizo zitatangazwa wazi na wahalifu kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kutozwa faini, kufungwa jela na hata mashirika ya uchapishaji kufungwa kabisa. 383680
captcha