Mjumbe wa Baraza la Usimamizi wa Haram ya Imam Hussein (as) Karim al Anbari amesema kuwa milango ya Haram hiyo imepanuliwa zaidi kwa ajili ya kuwawezesha wafanyaziara kufanya ibada zao kwa wepesi kutokana na kuongezeka idadi ya watu wanakwenda Karbala kuzuru kaburi la mjukuu huyo wa Mtume Muhammad (saw).
Al Anbari amesema kuwa uwanja wa haramu hiyo pia umepanuliwa zaidi na idadi ya milango ya kuingilia kwenye Haram ya Imam Hussein imeongezeka.
Idadi ya wafanyaziara wa Haram ya mjukuu wa Mtume Muhammad (saw) na bwana wa vijana wa peponi Imam Hussein (as) imeongezeka kwa kiwango kikubwa kufuatia koboreka hali ya usalama nchini Iraq hususan katika miji mitakatifu ya Karbala na Najaf. 383691