IQNA

Duru za mafunzo kwa maimamu wa misikiti ya Malaysia

11:53 - April 08, 2009
Habari ID: 1761939
Duru za mafunzo kwa maimamu wa misikiti nchini Malaysia zitaanza kutekelezwa kuanzia mwezi Julai huko katika mji wa Selangor.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Bernama, lengo la kuanzishwa duru hizo za masomo ni kuwaandaa maimamu wa miskiti ili wapate kutoa mafunzo bora ya Qur'ani kwa walio na hamu ya kujua mafundisho ya kitabu hicho kitakatifu.
Kunyanyuliwa kiwango cha masomo ya Kiislamu na hasa katika uwanja wa kuhifadhi Qur'ani Tukufu na kulea wataalamu wa tafsiri ya kitabu hicho cha wahyi ni malengo mengine ya duru hizo za masomo.
Duru za masomo hayo ambayo yataendeshewa katika Kituo cha Mafunzo ya Kusoma na Kuhifadhi Qur'ani cha Selangor zimedhaminiwa na Kundi la Ustawi la Kiislamu na Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Malaysia. 384278
captcha