IQNA

Msafara wa uhuru kwa ajili ya kukomesha mzingiro, wawasili Gaza

17:10 - April 08, 2009
Habari ID: 1762205
Msafara uliopewa jina la Msafara wa Uhuru wa Kamati ya Kukomesha Mzingiro wa Gaza umewasili katika eneo la Ukanda Gaza kwa ajili ya kukomesha mzingiro wa Wazayuni dhidi ya wakazi wa eneo hilo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kukomesha Mzingiro wa Gaza Adel Zaarab amesema kuwa kamati hiyo ina kamati tanzu 35 ndani ya Palestina na nchini Lebanon ambazo zinasaidia utekeleza wa mpango huo.
Zaarab amesema, msafara huo unajumumuisha meli kadhaa kutoka nchi za Kiarabu, Ulaya na Afrika. 383925
captcha