Ripoti zinasema kuwa watu wanaoswali katika misikiti hiyo wamekuwa wakiswali kwa kuelekea upande usiokuwa sahihi kutokana na ujenzi mbaya wa misikiti hiyo.
Al Kaaba ni eneo takatifu kwa Waislamu wote duniani na mihrabu zote za misikiti zinapaswa kuelekezwa upande wa nyumba hiyo tukufu ya Mwenyezi Mungu.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Saudi Arabia, mihrabu za misikiti hiyo hazikuelekezwa vizuri upande wa kibla.
Watu wanaoishi katika majumba marefu ya Makka wamegundua kuwa mihrabu za misikiti ya kale ya Makka hazikuelekezwa upande wa kibla. Waislamu wanaotumia misikiti hiyo wametoa wito wa kurekebishwa nakisi hiyo kwa kutumia vyombo vya kisasa.
Afisa mmoja wa Wizara ya Masuala ya Kiislamu ya Saudi Arabia amesema hilo si kosa kubwa na kwamba zimechukuliwa hatua za kusahihisha makosa hayo. 383904