IQNA

Isesco kushiriki katika kikao cha Uislamu na Ijtihadi nchini Ufaransa

12:03 - April 09, 2009
Habari ID: 1762313
Kikao cha kimataifa cha 'Uislamu na Juhudi kwa ajili ya Kufungamana na Zama: Maudhui ya Ijtihadi' ambacho kimeandaliwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni wa Kiislamu Isesco, kimefanyika Jumatano ya jana katika makao makuu ya Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa Unesco huko mjini Paris Ufaransa.
Wasomi na wanafikra wa Kiislamu na wasiokuwa Waislamu wanaoshiriki katika kikao hicho ambacho kimeandaliwa kwa ushirikiano wa Chuo cha Sheria cha Paris, Taasisi ya Usimamizi wa Utafiti wa Jografia ya Kisiasa ya Paris na Shirika la Kimataifa la Sheria wamajadili na kubadilishana mawazo kuhusu ijtihadi na matatizo yake katika jamii ya leo na nafasi yake katika matukio mbalimbali ya kijamii na kimataifa.
Abdul Aziz al-Tuwaijri, Katibu Mkuu wa Isesco atakuwa miongoni mwa watu waliozungumza katika kikao hicho ambacho kimeandaliwa katika fremu ya kuuarifisha Uislamu na kurekebisha sura ya dini hiyo iliyopotoshwa na baadhi ya watu ulimwenguni.
Wahadhiri na wanazuoni kutoka nchi za Saudi Arabia, Algeria, Misri, Imarati, Ufaransa, Lebanon, Morocco na Sudan ni baadhi ya watu walioalikwa kushiriki katika kikao hicho cha kimataifa. 384837
captcha