Msemaji wa Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu ya Uswisi Farhad Afhshar amesema kuwa kituo hicho kitakuwa na jumba la makumbusho la Kiislamu, msikiti, kumbi za mikutano ya Kiislamu na hoteli ya nyota nne.
Amesema kuwa ujenzi wa kituo hicho unahitaji bajeti ya franc milioni 80 na kwamba wahandisi mashuhuri wa majengo wamealikwa kuwasilisha ramani zao.
Afshar ameongeza kuwa mikutano ya kidini itakuwa ikifanyika katika kituo hicho kwa ushirikiano wa Waislamu wa Uswisi. 384943