Chuo Kikuu cha al Azhar kilikuwa tayari kumelitahadharisha jarida hilo kuhusu tabia ya kuchapisha makala zinazovunjia heshima matukufu ya Kiislamu lakini wamiliki wa jarida hilo walipuuza tahadhari hiyo.
Mahakama ya Misri imelitambua shairi lililochapishwa na jarida la Ibda' kuwa linamvunjia heshima Mwenyezi Mungu Mtukufu na kuamuru lisimamishwe mara moja. Mahakama hiyo imesema, uhuru wa habari hauna maana ya kuvunjia heshima mafundisho ya dini. Imesisitiza kuwa ukosoaji unapaswa kuwa na hoja za kimantiki na kuheshimu misingi ya jamii ya Kiislamu ya Misri.
Vilevile Chuo Kikuu cha al Azhar kimewasilisha mashtaka mahakamani dhidi ya mwandishi wa shairi hilo Hilmi Salim ambaye kimemtuhumu kuwa amemvunjia heshima Mwenyezi Mungu na dini ya Kiislamu. 385673