Jumuiya ya Waandishi Huru wa Habari ya Denmark imetangaza kuwa imeanza kuuza kibonzo hicho kinachomvunjia heshima Mtume wa Uislamu katika mtandao wa intaneti.
Viongozi wa jumuiya hiyo wametangaza kuwa kila nakala moja ya kibonzo hicho inauzwa kwa dola 250 sawa na Euro 188.
Nakala zote zinazouzwa zimetiwa saini na Westergad ambaye ni miongoni mwa wachoraji wa vibinzo 12 vilivyochapishwa mwaka 2005 za kukabiliwa na malalamiko makubwa ya Waislamu kote duniani.
Kibonzo hicho kinachomvunjia heshima Mtume Muhammad (saw) kimeanza kuuzwa huko Denmark katika hali ambayo Waziri Mkuu wa nchi hiyo Anders Fogh Rasmussen ambaye amechaguliwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa Shirika la Kujihami la Nchi za Magharibi NATO siku chache zilizopita alisema kuwa shirikila hilo limeazimia kuanzisha ushirikiano mpya na ulimwengu wa Kiislamu na kuheshimu wafuasi wa dini mbalimbali. 385595