IQNA

Mkutano wa kimataifa wa utalii wa Kiislamu kufanyika Malaysia

0:07 - April 12, 2009
Habari ID: 1763330
Mkutano wa Kimataifa wa Utalii wa Kiislamu, Hija na Umra umepangwa kufanyika tarehe 14 Aprili nchini Malaysia.
Mkutano huo utahudhuriwa na wataalamu 200 wa masuala ya utalii kutoka nchi mbalimbali, jumuiya za utalii za nchi za Kiislamu na taasisi zisizokuwa za serikali.
Miongoni mwa malengo ya mkutano huo wa kimataifa ni kuhuisha utalii kwa mujibu wa sheria za Kiislamu, kujadili njia za uwekezaji katika sekta hiyo na juhudi za kutangaza utalii wa Kiislamu kwa nchi zisizokuwa za Kiislamu.
Mwakilishi wa shirika la utalii la Malaysia Jafry Sulaiman amesema kuwa malengo mengine ya mkutano huo ni kuwahamasisha Waislamu kufanya safari za kitalii na kwamba mkutano huo pia utajadili ibada za hija na umra kama safari muhimu za Kiislamu. 385737
captcha