IQNA

Nd'jamena, mji mkuu wa utamaduni wa Kiislamu barani Afrika mwaka 2009

12:25 - April 12, 2009
Habari ID: 1763542
Sherehe za kuchaguliwa Nd'jamena, mji mkuu wa Chad kuwa mji mkuu wa utamaduni wa Kiislamu barani Afrika kwa mwaka huu wa 2009 zimefanyika mjini humo.
Mwakilishi wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ISESCO limetangaza kuwa mwakilishi wake ameshiriki katika sherehe hizo kwa mwaliko wa Waziri wa Utamaduni na Vijana wa Chad.
Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu pia limeutangaza mji wa Qayrawan nchini Tunisia kuwa mji mkuu wa utamaduni wa Kiislamu katika ulimwengu wa Kiarabu na miji ya Baku Azerbaijan na Kuala Lumpur Malaysia kwa pamoja kuwa miji mikuu ya utamaduni wa Kiislamu barani Asia katika mwaka huu wa 2009. 385987
captcha