IQNA

Kumalizika mashindano ya kitaifa ya kuhifadhi Qur'ani nchini Malaysia

16:04 - April 12, 2009
Habari ID: 1763776
Mashindano ya kitaifa ya kuhifadhi Qur'ani yaliyokuwa yakifanyika katika mji wa Kota Baharu nchini Malaysia yamemalizika kwa mafanikio na washindi kutunukiwa zawadi.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Bernama Mashindano hayo yalifanyika katika sehemu mbili za kuhifadhi Qur'ani nzima, juzuu ya kwanza hadi ya 15 kwa ajili ya makundi mawili ya wanawake na wanaume, ambapo washindi walipewa zawadi za fedha taslimu na kusaidiwa gharama za safari ya hija.
Kuhusiana na suala hilo, gavana wa jimbo la Kelantan aliwataka Waislamu katika sherehe za kuhitimisha mashindano hayo kutegemea mafundisho ya Qur'ani na sira ya maisha ya Mtume Mtukufu (saw) kwa ajili ya kutatua matatizo yao maishani. Amesema kuwa katika miaka ya hivi karibuni, Waislamu wamekuwa wakikabiliwa na matatizo na changamoto muhimu zinazotokana na Waislamu kuruhusu hitilafu zao za kiitikadi na kifikra kuwatawala, jambo ambalo baadhi ya wakati limeleta mgawanyiko na mvutano miongoni mwao.
Amesisitiza kwamba iwapo Waislamu watafuata na kutekeleza kivitendo sira ya Mtume Mtukufu (saw) bila shaka watafikia maendeleo makubwa badala ya kujishughulisha na masuala yanayozusha hitilafu na mgawanyiko kati yao. 386288
captcha