IQNA

Jarida la kwanza la kimataifa la 'Utafiti wa Kiislamu' lachapishwa

16:05 - April 12, 2009
Habari ID: 1763777
Jarida la kwanza la kimataifa la Utafiti wa Kiislamu linalotayarishwa na Chuo Cha Mafunzo ya Kidini na Utafiti wa Kiislamu cha Qatar limechapishwa nchini humo.
Kwa mujibu wa Gazeti la ar-Rayya la Qatar, Jarida hilo limechapishwa kwa ushirikiano wa wahadhiri wa chuo hicho na wataalamu kadhaa wa ulimwengu wa Kiislamu.
Kama linavyojieleza lenyewe, jarida hilo linachunguza na kuwasilisha makala mbalimbali kuhusiana na masuala na mafundisho ya Qur'ani Tukufu. Baadhi ya mambo yaliyojadiliwa humo ni pamoja na mapenzi katika Qur'ani Tukufu, kukaririwa baadhi ya mambo katika Qur'ani, ujumbe na utume na muujiza wa Qur'ani na uchunguzi wake katika kipindi chote cha historia ni baadhi ya masuala hayo.
Katika sehemu nyingine, jarida hilo linachunguza kwa kina umuhimu wa kutafuta elimu katika mafundisho ya Kiislamu na hasa kuhusiana na hadithi za Mtume Mtukufu (saw).
Jarida hilo linasema mwishoni mwa kurasa zake kwamba Qur'ani na sunna za Mtume ndizo zilizoanzisha misingi ya mwanzoni kabisa ya elimu na utafutaji elimu. 386346
captcha