Kitabu hicho ambacho anwani yake kamili ni, Jihadi ya Siri; Jinsi Uislamu Wenye Itikadi Kali Marekani Unavyotoweka Bila Kutumiwa Mabomu, kilichoandikwa na Mmarekani Robert Spencer kimekuwa kikisambazwa bure na jarida la Human Events miongoni mwa wasomaji wake. Katika kitabu chake hicho kilicho dhidi ya Uislamu Spencer anadai kwamba Uislamu unaenezwa nchini Marekani na makundi ya jihadi kwa lengo la kuitokomeza nchi hiyo kwa njia isiyo ya moja kwa moja na bila ya kutumiwa mabomu.
Robert Spencer ni miongoni mwa Wakristo wenye misimamo mikali na ya chuki dhidi ya Uislamu nchini Marekani ambaye hadi sasa ameandika vitabu vingi vinavyolenga kudhalilisha na kuutusi Uislamu na Mtume Muhammad (saw).
Baadhi ya vitabu vya mwandishi huyo mwenye chuki dhidi ya Uislamu ni pamoja na Uhakika wa Muhammad, Muasisi wa Dini Yenye Taasubi Kubwa Zaidi Duniani na Ukweli Kuhusu Muhammad; Muasisi wa Dini Yenye Itikadi Kali Zaidi Duniani.
Gazeti la Marekani la Human Events pia mwaka uliopita lilisambaza bure vitabu hivyo vya matusi dhidi ya Uislamu miongoni mwa wasomaji wake. 386761