IQNA

Muhammad (saw), kiongozi mkubwa zaidi wa kisiasa duniani

13:38 - April 13, 2009
Habari ID: 1764146
Michael Hart, mwandishi wa Marekani ameashiria vita vingi vilivyoongozwa na Mtume Muhammad (saw) mwanzoni mwa Uislamu na kusema kuwa jambo hilo linamfanya Mtume kuwa kiongozi mashuhuri na mkubwa zaidi wa kisiasa katika kipindi chote cha historia ya mwanadamu.
Kwa mujibu wa tovuti ya Muhit, Michael Hart amesema kuwa Mtume Muhammad aliweza kuasisi na kusambaza duniani moja ya dini kubwa zaidi kupitia ujumbe aliokuja nao na hivyo kubakisha katika jamii mbalimbali athari za ujumbe wake ambazo zinazidi kuenea hata baada ya kupita karne 13 tokea kuasisiwa dini hiyo tukufu.
Amesema, kama alivyokuwa Nabii Isa (as) Mtume aliweza kuiathiri kwa kiwango kikubwa jamii ya mwanadamu isipokuwa kwa tofauti hii kwamba, mbali na Mtume Muhammad kuwa kiongozi wa ujumbe wa mbinguni alikuwa pia kiongozi wa masuala ya kidunia.
Mwandishi huyo wa masuala ya fizikia na nujumu ambaye hutumia dalili za Qur'ani katika uandishi wa vitabu vyake vya utafiti, anaamini kwamba sifa za Mtume Muhammad (saw) hazina mfano wake katika historia kutokana na kuwa jina na shakhsia yake ndiyo ya pekee ambayo itaendelea kudumu milele katika jamii ya mwanadamu. 386676
captcha