IQNA

Kumalizika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani nchini Saudi Arabia

14:02 - April 13, 2009
Habari ID: 1764150
Duru ya tano ya mashindano ya kimataifa ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu, maalumu kwa wanajeshi na yaliyopewa jina la Zawadi ya Kimataifa ya Amir Sultan bin Abdul Aziz yalimalizika siku ya Jumamosi katika mji mtakatifu wa Makka kwa kuandaliwa sherehe maalumu.
Mashindano hayo ya wiki moja yaliyoanza Jumamosi tarehe nne Aprili yalisimamiwa na Amir Sultan bin Abdul Aziz, Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudi Arabia na kuwashirikisha washindani 69 kutoka nchi 19 za Kiarabu na Kiislamu.
Washindani walishiriki katika mashindano hayo kwa kuhifadhi Qura'ni nzima, juzuu 20, juzuu 10 na juzuu tano kwa mbinu ya tajweed.
Abdallah bin Swaleh Aal Sheikh mmoja wa wasimamizi wa mashindano hayo amesema kuwa maonyesho ya Usalama wa Kifikra yamefanyika pambizoni mwa mashindano hayo ili kuonyesha juhudi zinazofanywa na Saudi Arabia katika kusambaza mafundisho ya Kiislamu duniani. Zawadi nono zimetolewa kwa washindi waliofanikiwa kupata nafasi nzuri katika mashindano hayo. 386649
captcha