Maudhui zinazopaswa kuchambuliwa na kujadiliwa katika ripoti hizo ni pamoja na, kumsubiri mwokozi; mapambano ya Kiislamu na mustakbali wa ulimwengu, fakihi mtawala na mapambano tokea Ashura hadi leo, taswira ya mapambano ya Kiislamu katika ulimwengu wa leo, kulaaniwa kimya cha serikali za Kiarabu kuhusiana na kukandamizwa kwa harakati za Kiislamu ulimwenguni na kupotoshwa kwa sura halisi ya harakati ya mapambano ya Kiislamu na vyombo vya habari vya Magharibi na Wazayuni na Mawahabi.
Malengo ya tamasha hilo yametajwa kuwa ni kumuarifisha Imam Mahdi (af) ulimwenguni, kubainisha siasa za mfumo wa Kiislamu wa Iran katika kumuarifisha mwokozi huyo halisi wa jamii ya mwanadamu katika kukabiliana na madai ya uongo ya nchi za Magharibi zinazodai kuwa ndio wakozi wa wanadamu, kuandaa mazingira ya kudhihiri mwokozi Imam Mahdi (af) kuzisaidia taasisi na mashirika ya serikali na yasiyo ya serikali yanayoshughulikia suala la mwokozi wa mwisho kupitia uimarishwaji wa vyombo vya habari na upashaji habari, kuimarisha moyo wa matumaini na msisimko miongoni mwa watu kuhusiana na suala la mwokozi wa mwisho, kuchambuiwa fikra za wasomi mbalimbali kuhusiana na Imam Mahdi na nafasi ya mapinduzi yake katika kuimarisha tauhidi na uadilifu katika jamii.
Walio na hamu ya kuwasilisha makala na utafiti wao kuhusiana na suala hilo wanaweza kufanya hivyo kupitia anwani ifuatayo: www.lsf.ir au kupitia simu zifuatazo: 22166315, 2217731, 22166302, 22166404 na 22013800. 387482