IQNA

At-Tuweijiri na Amr Musa wajadili njama za Mayahudi huko Quds

9:22 - April 15, 2009
Habari ID: 1765106
Abdul Aziz Othman al-Tuwaijri, Katibu Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu Isesco amekutana na kubadilishana mawazo na Amr Musa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kuhusiana na njia za kukabiliana na njama za utawala haramu wa Israel za kubadili muundo wa kijamii wa eneo la Baitul Muqaddas kwa manufaa ya Mayahudi.
Kwa Mujibu wa Isesco, pande mbili hizi zimejadili njia za kuimarisha ushirikiano wao katika nyanja za mazungumzo kati ya tamaduni, staarabu, kuimarisha elimu katika nchi za Kiarabu na kukabiliana vilivyo na njama za Israel za kuondoa utambulisho wa Kiislamu na Kiarabu wa mji wa Quds Tukufu na kutaka kuufanya uonekane kuwa ni wa Kiyahudi.
Mwishoni mwa mazungumzo hayo, Katibu Mkuu wa Isesco alimwalika Amr Musa kushiriki katika kikao cha kimataifa cha mazungumzo kati ya staarabu na tamaduni tofauti ambacho kimepangwa kufanyika hivi karibuni katika mji wa Qayrawan huko Tunisia.
Mwaka 1967 utawala ghasibu wa Israel uliuteka kikamilifu mji wa Baitul Muqaddas na tokea wakati huo umekuwa ukitekeleza miradi na mipango haribifu ya kufuta kabisa utambulisho wa Kiislamu na Kiarabu wa mji huo kwa kubomoa na kuharibu kabisa nyumba na majengo ya Waarabu wa Kipalestina na kujenga vitongoji vya Mayahudi sehemu yake. 388071
captcha