IQNA

Mbinu mpya ya maadui wa Uislamu wa Tunisia dhidi ya Qur'ani

9:10 - April 15, 2009
Habari ID: 1765112
Katika hatua moja ya kiburi na jeuri, kundi moja la Watunisia walio na uadui dhidi ya kitabu kitakatifu cha Qur'ani wanatumia mbinu mpya kupitia tovuti ya mazungumzo ya Facebook katika kutusi na kukidharau moja kwa moja kitabu hicho cha mbinguni na matukufu mengine ya Waislamu.
Kwa mujibu wa gazeti la tovuti la Sabq, Watunisia hao ambao ni wa mrengo wa kushoto wanaopinga mafundisho ya dini, wametoa matusi makubwa kupitia mtandao wa Facebook dhidi ya Mwenyezi Mungu, Mtume Wake (saw) na matukufu mengine ya kidini na hasa Qur'ani Tukufu.
Chini ya anwani, "Baada ya Vikaragosi vya Denmark…. Sasa ni Kurasa za Facebook ya Watunisia", gazeti la al-Arab limeandika kuwa makundi ya kisiasa na Kiislamu ya Tunisia yamekuwa yakishiriki kwa wingi katika mijadala ya matusi na dharau dhidi ya matukufu ya Kiislamu kwa kisingizio cha uhuru wa kusema na kujieleza.
Gazeti hilo vilevile linasema kuwa hujuma hiyo dhidi ya Uislamu bado inaendelea na hata baadhi ya wahadhiri wa vyuo vikuu na vituo muhimu vya kielimu akiwemo Ulfat Yusuf, mhadhiri wa masuala ya historian a Utamaduni, wanaonekana miongoni mwa watu hao wanaotusi wazi matukufu ya Kiislamu na hasa Mtume Mtukufu (saw). 388165
captcha