IQNA

Mafundisho ya Kiislamu yanapaswa kuwa ya kisasa

12:31 - April 16, 2009
Habari ID: 1765622
Waziri wa Masuala ya Kidini wa Malaysia amesema katika kikao cha Elimu ya Juu ya Kiislamu kwamba kuna haja kubwa ya kufanyika marekebisho katika mfumo wa elimu na mafundisho ya Kiislamu.
Kwa mujibu wa shirka la habari la Bernama, Waziri Jamil Kheir Baharom amesema kuwa watafiti na wataalamu wa masuala ya Kiislamu wanapaswa kubuni mifumo mipya ya elimu na masomo kwa namna ambayo itaweza kukidhi haja na mahitaji ya jamii ya leo ya Kiislamu. Amesema kuwa iwapo mipango na mifumo hiyo itarekebishwa ni wazi kuwa takuwa na taathira katika ubora wa masomi katika ulimwengu wa Kiislamu na hivyo kuharakisha mwenendo wa ustawi katika nchi za Kiislamu.
Waziri wa Masuala ya Kidini wa Malaysia amesisitiza kwamba serikali ya nchi hiyo iko tayari kusaidia utekelezwaji wa mipango kama hiyo ya kuboresha mifumo ya mafunzo ya Kiislamu nchini.
Iwapo mipango hiyo itatekelezwa, masomo mengine kama vile sheria za Kiislamu, mifumo ya benki za Kiislamu masuala yanayohusiana na chakula katika Uislamu yataingizwa katika mipango hiyo.
Wawakilishi wa mashirika na taasisi za mafunzo ya juu ya kidini kutoka nchi za Indonesia, Ufilipino, Brunei na Thailand wameshiriki katika kikao hicho kilichofanyika nchini Malaysia. 388918
captcha