IQNA

Wilders kutengeneza sehemu ya pili ya filamu ya Fitna

15:52 - April 20, 2009
Habari ID: 1765983
Geert Wilders, mwanasiasa na mbunge mwenye siasa za kufurutu mipaka wa Uholanzi amesema kuwa atatengeneza sehemu ya pili ya filamu ya Fitna inayotusi matukufu ya Kiislamu hususan kitabu kitakatifu cha Qur'ani.
Amesema kuwa katika sehemu hiyo, atabainisha athari za Uislamu katika nchi za Magharibi. Wilders ametabiri kwamba filamu hiyo ambayo anatazamia kuikamilisha mwishoni mwa mwaka 2010 itaamsha hasira kubwa ya Waislamu ulimwenguni kama ilivyofanya sehemu ya kwanza ya filamu hiyo ya kichochezi.
Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 45 na aliye na chuki ya kupindukia dhidi ya Uislamu, ameamua kutengeneza filamu hiyo ya matusi na dharau dhidi ya Uislamu katika hali ambayo mwaka jana mahakama moja ya Uholanzi ilimpata na kosa la kuchochea hitilafu miongoni mwa mataifa kwa kutengeneza filamu Fitna inayomtusi Mtume (saw) na Qur'ani na kudharau matukufu ya Kiislamu. 389535
captcha