IQNA

Televisheni mpya ya kidini ya satalaiti kuanzishwa nchini Tunisia

9:15 - April 18, 2009
Habari ID: 1765985
Televisheni mpya ya kidini inayorusha hewani matangazo yake kupitia mitambo ya satalaiti, inayoitwa Zeituna itazinduliwa hivi karibuni nchini Tunisia.
Kwa mujibu wa tovuti ya Nasij, mpango wa kutayarisha urushaji hewani wa matangazo ya televisheni hiyo unasimamiwa na Swakhr al-Matari.
Televisehni hiyo itakuwa ikirusha hewani vipindi mbalimbali vya kidini vinavyowavutia watazamaji wake.
Televisheni ya kwanza ya aina hiyo inayoitwa Hanibaal Firdaus ilizinduliwa nchini humo mwezi Ramadhani mwaka uliopita na redio ya Zeituna pia kuzinduliwa mwaka huohuo.
Swakhr al-Matari ni mmoja wa wafanyakazi wa Tunisia ambaye alizindua redio ya Qur'ani iliyotajwa na pia ana mipango ya kuanzisha benki ya Kiislamu nchini humo. 388436
captcha