IQNA

Maandamano ya Wapalestina dhidi ya Israel katika Msikiti wa al-Aqsa

15:52 - April 20, 2009
Habari ID: 1765986
Wananchi wa Palestina wamefanya maandamano makubwa ya kupinga vitendo vya uharibifu na dharau vinavyotekelezwa na utawala haramu wa Israel katika Msikiti Mtukufu wa al-Aqsa na njama za utawala huo za kujaribu kufuta utambulisho wa Kiislamu na Kiarabu wa eneo la msikiti huo.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Kuwait KUNA, maandamano hayo yamefanyika kufutia wito uliotolewa na harakati pamoja na makundi ya Kiislamu ya Baitul Muqaddas kwa ajili ya kutetea na kuulinda msikiti huo kutokana na uharibifu wa magenge ya Kiyahudi na Kizayuni yenye misimamo ya kupindukia mipaka yanayotaka kuharibu kabisa utambulisho wa Kiislamu wa msikiti huo.
Askari ghasibu wa Israel wamechukua hatua kali za kiusalama kwa ajili ya kuwazuia Wapalestina kuingia katika msikiti huo mtakatifu. Askari hao waliwatia nguvuni Waislamu waliopuuza hatua hizo za kiusalama na kuingia katika msikiti huo kwa ajili ya kutekeleza ibada zao kwa mujibu wa mafundisho ya dini yao tukufu ya Kiislamu.
Askari wa utawala huo pia waliwazuia Wapalestina wa Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan waliokuwa na nia ya kwenda kutekeleza ibada zao katika msikiti huo ulioko Beitul Muqaddas. 389685
captcha