IQNA

Allamah Fadhlullah:

Kuikomboa Palestina ndio lengo kuu la harakati za mapambano

12:06 - April 19, 2009
Habari ID: 1766794
Mwanazuoni mashuhuri wa Kiislamu wa Lebanon Allamah Muhammad Hussein Fadhlullah amesema kuwa ni fahari kubwa kwa makundi ya mapambano ya Palestina na Lebanon kuwasaidia wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina na akasisitiza kuwa suala la ukombozi wa Palestina ndiyo lengo kuu la makundi hayo.
Allamah Fadhlullah amelaani vikali kimya cha ulimwengu wa Kiarabu mbele ya jinai zinazoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni wa Isrel katika msikiti wa al Aqsa.
Amesema, katika cha huko nyuma hadi hivi sasa suala la Palestina limekuwa likinyamaziwa kimya na watu waovu na dhaifu na kupiganiwa na wanajihadi shupavu wenye ikhlasi na wakweli.
Allamah Fadhlullah amesema kuwa utendaji wa wanamapambano wa Palestina umeupa changamoto mbili ulimwengu wa Kiarabu ambazo ni ama kufanya jitihada za kuikomboa Palestina au kulitupilia mbali suala hilo. Amesema tawala nyingi za Kiarabu zimehitari njia ya pili ya kulipuuza suala la Palestina.
Ayatullah Fadhlullah amesema kuwa tatizo kubwa linalozikabili nchi za Kiarabu ni kadhia ya Palestina na kujisahaulisha haki ya kuikomboa nchi hiyo inayokaliwa kwa mabavu na Wazayuni. Amelaani vikali kimya cha ulimwengu wa Kiarabu mbele ya jinai za Israel huko Masjidul Aqsa na jinai nyingine za utawala wa Kizayuni na akasema kuwa baadhi ya makundi ya Kiarabu yanataka kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel huku ulimwengu wa Kiislamu ukiendelea kushuhudia koporwa ardhi zaidi za Palestina katika operesheni za ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi. 390068

captcha