Kwa mujibu wa tovuti ya Tradechakra, kikao hicho kimeandaliwa na Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Malaysia na Benki ya Ustawi wa Kiislamu kwa lengo la kuimarisha uchumi wa Kiislamu. Uchumi wa Kiislamu, masuala ya benki za Kiislamu, uchumi wa nchi za Kiislamu wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC, ushirikiano wa kiuchumi miongoni mwa nchi wanachama wa OIC na mafunzo kuhusiana na masuala ya kifedha na uchumi wa Kiislamu ni miongoni mwa masuala yaliyopangwa kujadiliwa katika kikao hicho. 390085