IQNA

Isesco yalaani uharibifu wa Wazayuni katika Msikiti wa al-Aqsa

16:27 - April 19, 2009
Habari ID: 1766962
Kikao cha pili cha wataalamu wa masuala ya historia na ya kale wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ISESCO ambacho kilifanyika siku ya Ijumaa huko Jordan kimelaani vikali hatua za maghasibu wa Kizayuni wanaochimba njia za chini kwa chini pambeni na katika msikiti mtakatifu wa al-Aqsa.
Gazeti la ad-Destur la Jordan limeandika kuwa, wataalamu hao ambao wamekuwa wakikutana huko Amman tokea siku ya Alkhamisi wameutaka utawala haramu wa Israel kusimamisha mara moja uchimbaji huo ambao unakiuka sheria na mapatano yote ya kimataifa. Wamezitaka nchi wanachama wa OIC kutoa mchango wao wa kimaada na kisanaa kwa Wizara ya Utalii na Athari za Kihistoria ya Palestina na wakati huohuo kutuma ujumbe nchini Palestina kwa shabaha ya kulinda na kukarabati athari za kihistoria na Kiislamu za mji mtakatifu wa Quds. Wataalamu wa kimataifa wa atahri za kale na kihistoria wamekuwa wakikutana mjini Amma kwa lengo kuchunguza hali ya mji mtakatifu wa Quds, pendekezo la Jordan kuhusiana na Babul Maghariba na kutazama upya ripoti za kisheria kuhusiana na marufuku ya kuchimbwa pembeni mwa Msikiti wa al-Aqsa. 390447
captcha