Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la Yemen, Sabanews, kikao hicho cha siku moja kitajadili masuala mbalimbali yanayohusiana na wanawake yakiwemo ya haki za wanawake katika kubuniwa sheria za Kiislamu na jinsi ya kuzuia kuvunjika kwa familia. Hotuba kuhusiana na mada hii ya mwisho itatolewa na Atiq Abdallah al-Hamidi, mwanachama wa Jumuiya ya Wanazuoni wa Yemen.
Akizungumza na shirika hilo la habari, Iman Abdulrahman Ar-Ridhaa, Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake wa Yemen amesema kuwa lengo la kufanyika kikao hicho ni kuwafahamisha wanawake wa nchi hiyo, nyadhifa, majukumu, nafasi na haki zao kwa msingi wa mafundisho ya dini tukufu ya Kiislamu. Amesema lengo jingine ni kuwahamasisha wanawake kufuatilia haki zao za kisiasa, kijamii na kiuchumi katika jamii za Kiislamu. 390857