Shule hiyo imefunguliwa na Taasisi ya Kuhifadhi Qur'ani ya Haraa.
Kwa mijibu wa tovuti ya Bokra.net, shule hiyo ilifunguliwa siku ya Jumamosi katika sherehe maalumu zilizohudhuriwa na wahudumu pamoja na wakuu wa masuala ya Qur'ani na kwa hotuba ya Raid Fat'hi msomi na mtafiti wa Kipalestina.
Jina la shule hiyo linatokana na shahidi wa eneo hilo Amir Mahmoud Khalayila ambaye aliuawa mwaka jana na askari ghasibu wa Israel akiwa na umri wa miaka 16 tu. 390840