IQNA

Maandamano makubwa dhidi ya Israel yafanyika mjini Geneva

9:24 - April 20, 2009
Habari ID: 1767072
Maelfu ya watu wamefanya maandamano makubwa mjini Geneva Uswisi dhidi ya utawala haramu wa Israel na siasa zake za kibaguzi dhidi ya Wapalestina kabla ya kuanza kikao cha kimataifa cha kupinga ubaguzi mjini humo.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Kuwait KUNA, maandamano hayo yameandaliwa na mashirika yasiyo ya kiserikali ya nchini Uswisi kwa ushirikiano wa mashirika kama hayo ya nchi za Kiarabu na Kiafrika kwa lengo la kulaani hatua za kiukandamizaji za Isreal na pia siasa za kibaguzi zinazotekelezwa katika pembe mbalimbali za dunia.
Kikao cha kupinga ubaguzi wa rangi cha Umoja wa Mataifa ambacho kimepangwa kujadili utendaji na mipango ya umoja huo katika kukabiliana na ubaguzi wa rangi duniani, kimeanza leo Jumatatu katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko Geneva na kimepangwa kuendelea hadi tarehe Nne Aprili.
Vilevile washiriki wa kikao cha Jamii ya Kirai mjini humo siku ya Ijumaa walitoa taarifa wakilaani vitendo vya unyanyasaji na ubaguzi wa rangi vinavyotekelezwa na utawala haramu wa Israel dhidi ya Wapalestina wasio na hatia wala ulinzi. 390727
captcha