IQNA

Tuwaijri awataka Waislamu kutetea Msikiti wa al-Aqsa

15:35 - April 21, 2009
Habari ID: 1768044
Abdul Aziz bin Othman al-Tuwaijri, Katibu Mkuu wa Shrika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ISESCO ametoa wito kwa nchi za Kiislamu akizitaka ziunge mkono na kutetea kwa kila njia Msikiti Mtukufu wa al-Aqsa dhidi ya uchumbaji haramu na haribifu unaofanywa na utawala haramu wa Israel katika msikiti huo na pia kukabiliana na njama zake za kulifanya eneo hilo takatifu kuwa na utambulisho wa Kiyahudu.
al-Tuwaijri amewataka Waislamu wote kuwa na umoja na mshikamano na kushirikiana katika kutetea matukufu yao katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala wa Israel na hasa Msikiti wa al-Aqsa.
Huku akisema kuwa Wazayuni wanatumia uungaji mkono wa nchi za Magharibi na fedha nyingi wanazopata kutoka kwa lobi za Kizayuni katika nchi hizo kwa ajili ya kudhibiti Msikiti wa al-Aqsa na Quds Tukufu, al-Tuwaijri amezitaka nchi za Kiislamu kuwa na umoja na kuvunja njama za Wazayuni kuhusiana na suala hilo.
Amesisitiza kuwa Wazayuni wanashirikiana kikamilifu na waungaji mkono wao kwa lengo la kudumisha vita dhidi ya Waislamu na akasema kuwa Wazayuni wamekuwa wakiwatumia vibaya Mayahudi kwa lengo la kupata uungaji mkono na himaya kutoka nchi za Magharibi na hivyo kuendelea kukanyaga haki za Wapalestina.
Katibu Mkuu wa Shrika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ameongeza kuwa Wazayuni wanendelea kukanyaga haki za Wapalestina kwa njia ambayo inadhihirisha siasa zao za kibaguzi na jinai dhidi ya watu wasio na hatia. 391538
captcha