IQNA

Mkutano wa waungaji mkono wa sheria ya Kiislamu nchini Somalia

15:46 - April 21, 2009
Habari ID: 1768048
Watu wapatao mia saba ambao ni waungaji mkono utekelezwaji wa sheria ya Kiislamu nchini Somalia wamekutana mjini Mogadishu, mji mkuu wa nchi hiyo kwa lengo la kujadili suala hilo.
Kwa mujibu shirika la habari la Ufaransa, washiriki wa mkutano huo ambao wengi walikuwa wamebeba picha ya Rais Sharif Sheikh Ahmad Sheikh wa nchi hiyo walikuwa wakipiga nara za kutaka amani na usalama wa kudumu nchini Somalia.
Tarehe 18 Aprili, Bunge la Somalia lilipitisha kwa sauti moja utekelezaji wa sheria za Kiislamu nchini Somalia, nchi ambayo imekuwa ikishuhudia mapigano makali kati ya makundi hasimu ya kikabila tokea mwaka 1991. 391429
captcha