IQNA

Mwanazuoni mashuhuri wa Kiislamu auawa na Wamagharibi Afghanistan

16:43 - April 21, 2009
Habari ID: 1768105
Mwanazuoni mashuhuri wa Afghanistan Maulawi Abdulqahir ameuawa katika shambulizi lililofanywa na ndege za kijeshi za nchi za Magharibi.
Mwandishi wa IQNA nchini Afghanistan ameripoti kuwa Rais Hamid Karzai wa nchi hiyo ametuma salamu za rambirambi kwa taifa la nchi hiyo akisisitiza kwamba atautaka uongozi wa vikosi vya askari wa kigeni nchini humo kutoa maelezo kuhusua mauaji hayo.
Rais Karzai amesema amesikitishwa mno na mauaji hayo na akazitaka Wizara za Ulinzi, Mambo ya Ndani na taasisi husika kuchunguza tukio hilo na kuwafuatilia wahusika. Amesema kuwa kuuawa kwa mwanazuoni huyo mkubwa ni hasara kubwa kwa jamii ya Afghanistan.
Sheikh Maulawi Abdulqahir alikuwa miongoni mwa maulamaa wakubwa wa Afghanistan katika mkoa wa Logar. Aliuawa Jumamosi iliyopita akiwa nyumbani kwake katika shambulizi la ndege za kivita za nchi za Magharibi. 391048

captcha