Mwenyekiti wa Umoja wa taasisi za Elimu za Kiislamu za Ivory Coast Kinate Abubaki amesema kuwa lengo la mkutano huo ni kujadili njia za koberesha elimu kwa wafuasi wa dini ya Kiislamu na kukuza kiwango chao cha elimu.
Amesema kuwa japokuwa taasisi hoyo inafanya kazi kwa kipindi cha miaka kumi na mbili sasa lakini haijafikia malengo yaliyokusudiwa.
Abubaki amezitaka jumuiya za serikali na za kimataifa kusaidia sekta ya elimu katika shule za Kiislamu nchini Ivory Coast na kusisitiza kuwa shule za Kiislamu za Ivory Coast zinahitajia misaada ya Wizara ya Elimu na Shirika la Unicef ili kufikia malengo yake. Amesema kuwa lengo la jumuiya hiyo ni kukiwezesha kizazi kijacho kufaidika na elimu bora. 391776